Social Items

PropellerAds

NJIA NZURI ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSNIANO YAKO


NJIA 7 NZURI ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO YAKO:

Kuna aina nyingi za mahusiano, yapo ya kirafiki, ya familia, ya kazini, kwenye mahusiano ya mwanamke na mwanaume na hata mahusiano ya mwanamke na mwanamke na ya  mwanaume na mwanaume yapo.
Kila mmoja anamahitaji yake ya kipekee  yanayomuelezea yeye kuwa  ni mahusiano gani  alionayo. Na ukumbuke binadamu tunahitaji kuelewana ili kuziimarisha roho zetu na miili yetu.lakini ukweli ni kwamba , kukosekana kwa mahusiano mazuri  humaliza  akili za watu na nguvu pia.
Hasa pale panapokuja swala la  ugumu  la mawasiliano. Ugumu wa mawasilinao unatokana na kutokufahamu njia nzuri ni zipi za kuwasiliana na mwenzako katika wakati husika.
Kwa ufupi  sifa ya kila mahusiano hushusishwa na sifa ya  mawasiliano.

Inabidi kujifunza kuwasiliana ambapo ndio njia nzuri ya kutengeneza mahusiano bora. .Kuzijua njia hizi kutakufanya uwe na mawasiliano bora na mahusiano bora

1.Jifunze kutulia.
Mruhusu mtu unaewasiliana nae kuongea jinsi anavyojisikia  na atoe mawazo yake bila ya wewe kumuingilia. Vaa kiatu chake wakati huo unaposikiliza,  hapo unaposikiliza hautakuwa tu unamwelewa bali utakuwa unajifunza na kupata uzoefu na uwelewa mzuri zaidi.
Usimkatize katize kwa kujitetea ama kumbeza mwache aseme. Hata kama kuna machozi ndani yake mwache alie. Mruhusu kuzungumza yote ili kukupa nafasi ya kuelewa . Lakini pia kupata nafas ya kujua nn kifanyike na kwa namana gani..

2.Jifunze kuwa msikilizaji mzuri.
Fanya kama wewe umealikwa  na unataka kuwasikiliza watu wanaowasiliana. Lakini usije ukakaa tu bila ya maswali. Jitahidi kuuliza maswali mengi ili kuongeza hari ya huyo mzungumzaji aendelee  kuongea, na wakati huo usitegemee majibu , Ila  kumbuka kuwa uko kwenye mawasiliano ya namna gani. Uwe makini na hilo ili usitoke nje ya mstari.
 kujifunza kusikilizza pia kutakufanya uweze kujenga utulivu na mazingira mazuri ya kuelewa kinachozungumzwa. hapa ondoa papara na uwe msikilizaji.

3.Wengine huvuta hisia za mwanzo.
Pamoja na kwamba utaweka nguvu ya kusikiliza , bado kuna watu  wanaopenda kukumbushia yalipita ili kuleta kitu cha kutoelewana. Wewe unyesha kujali bila kuogopa hayo, baadae yeye mwenyewe ataona haina haja ya kubaki na haya, na utaona itachukua muda mfupi tu kuelewana.


4.Usipanic, usifanye papara.
Mawasiliano yanapoendelea usiyaiingilie, subiri mpaka huyo mtu  anayeongea amalize kuongea.  na kujieleza.  Na kama utaona hayuko tayari kukusikiliza ama hayuko tayari kuendelea na mawasiliano hayo usilazimishe . Mpe muda tu kwa sababu ukilazimisha hutapata kile ulichotamani muwasiliane kwacho. Ni vyema kutoa muda, KUTOKUWA NA SHAKA na kumwacha aamue lini yuko tayari kuzungumza juu ya swala unalotaka muzungumze.

5.Usijaribu kuongea juu ya mtu mwingine.
Kama ulikuwa unaongea na ukaona  umeingiliwa katika maongezi yako , tulia,  usijaribu kuongea juu ya mtu mwingine, yaani mtu anaongea na wewe unaongea , usifanye hivyo. hatakujibu hata hivyo labda awe ni mtu wa ovyo, lakini kama hataweza  kuwasiliana vyema. jaribu tu kutoa nafasi kwa kila upande umsikilize mmoja baada ya mwingine . Kitendo cha kuingilia mazungumzo kinafanya mufungue mlango wa magomvi na hakutakuwa na maelewano kati yenu.

6.Wasaidie wengine wawe wasikilizaji wazuri pia.
Hii hapa inafanyika hivi, kama  umewaeleza kitu  uliza endapo wamekuelewa ulichowaambia, na wakueleze ulichokisema. na hapa ndipo utakapojua kuwa kuna wasikilizaji ama hakuna,lakini usiache kuwaelewesha  mpaka wamekuelewa.

7.Usihofie ukimya wa muda.
Wakati wa ukimya ndio wakati mzuri wa mawasiliano, hata hivyo katika hali nyingi za mawasiliano ya ukimya  unawafanya watu wasijiamini, wasitulie.

Lakini kumbuka kuna watu wanahitaji ukimya ili wakusanye mawazo yao ili wawe salama kuongea kitu cha msingi. na wakati huo wa ukimya unatakiwa kuwa msikilizaji mzuri zaidi ya wakati wa kuongea.


No comments