Social Items

PropellerAds

MITANDAO YA KIJAMII

MITANDAO YA KIJAMII
Mitandao ya kijamii. Wengi wetu tunaifahamu n tunaitumia kila iitwapo leo. Ipo mitandao mbalimbali ya kijamii kama  Facebook . Instalgram.  LinkedIn . Badoo.  N.k
Wengi wetu tunatumia mitandao ya kijamii kwa njia moja au nyingine . Wapo ambao wamebobea katika mambo mbalimbali katika mitandao hiyo n wanaitumia vizuri kulingana n ubobevu wao.

Nikuulize kama kijana mitandao hii ya kijamii inakusaidia nini katika maisha yako ..?

Lazima uwe na muda wa kutathimini ni kiasi gani unafaidika na mitandao hii ya kijamii. Usiitumie tu kwa vile unawez kutumia jiulize na ujipime

Vijana walio wengi mitandao hii wanitumia kwa ajili ya kupiga picha na kubadili pozi kila kulicha wengi tena picha mbaya za utupu wao kabisa.

Wengine hutumia kutazama picha za warembo waliko katika utupu.  Au kusikiliza miziki . Wengine kutazama fulani leo atakuwa n skendo gani. Kumfuatilia super star fulani. Kutafuta wapenz au wake kwa waume .Kutafuta umbea na vitu kama hivyo.  Hii ni mfano mchache tu ya matumizi ya wengi wetu.

Kila mmoja anapoweka fedha katika simu yake ili kupata nafasi ya kupakua na kusoma mambo mbalimbali katika mitandao hii ya kijamii. 

NIKUUKIZE JE KUNA FAIDA KAZI UNAIPATA KAMA KIJANA KWA KUTUMIA MTANDAO YA KIJAMII

Mitandao ya kijamii ni hazina kubwa sana y kujiongezea kitu kizuri maishani,   unaweza kuwa milionea mkubwa sana, ama  unaweza kuwa mtu fulani wa dhamani sana. Lakin  pia unaweza kuwa kituko cha kutisha katika jamii kwa sababu y mitandao hii

Itakunufaisha tu ukijua n jinsi gani unatakiwa kuitumia . Njia amabyo utatumia vyema na kwa jinsi gani utumie ikunufaishe . Jifunze basi usiwe na haja ya kusubiria kuambiwa tu jifunze leo

Ni wapi inapotumia mitandao ya kijamii kujinufaisha. ? N lazima ujue sehemu ambayo itakuwa na faida kwako na sio wewe uwe unaweka fedha tu unapoteza muda wako na bado hakuna unafaidika nalo.

Kwa ufupi kabisa kama wewe ni mfanyibiashara tumia vizuri mitandao hii ili upate faida na baishara yako ikue.
Kama wewe n mwalimu au mwanfunzi tumia vizur ili upate faida

Tangaza kazi zako  tangazo lako linaweza kuwafikia watu wengi sana kama utajua vyema jinisi ya kutumia mitandao ya kijamii.  Wengi wetu tunaona watu WALIOFANIKIWA tukafikiria vibaya labda wana jambo fulani baya lakin ukweli n kuwa hakuna kitu kinafanya kazi na kusambaza taarifa kwa haraka kama mitandao ya kijamii. 

Social capital ni ya muhimu sana katika maisha yako kama tu unataka kufanikiwa sana . Mimi nimefanikiwa kufanya baishara zangu hasa na network marketing kwa sbabu nilijua vyema jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii.

Pia kuza thamani yako ndani ya jamii yako kwa urahisi sana kupitia katika mitandao ya kijamii na hapo utaona umuhimu wa kutumia badala ya kuwa shimo la kula tu fedha zako sasa sehemu ya kukuzalishia fedha zaidi

Anza sasa kuwafuatilia wale wanafanya vitu unapenda kufanya angalia wanafanyaje n kutumiaje mitandao hii uone nawe unaweza kufanya nn katika eneo hilo.
Pia wafunze wenzako wailoko karibu nawe kuwa hii mitandao sio sehemu y matusi masengenyo, ugomvi n.k Bali n kama kiwanda cha kukuzalishia kile unataka.

Karibu tuendelee kufanya kazi pamoja katika mitandao y kijamii

Kwa leo nakusihi kama kijana chunguza faida ya mitandao ya kijamii kwa maisha yako na uchukue hatua  ya kujifunza . Acha kusoma anza kujaribu na utafanikiwa tu
Uwe na wakati mwema

1 comment:

  1. Ahsante sana mamy nimejifunza, maana tulio wengi simu tunazitumia kwa lengo la kuangalia vitu mtandaoni na kuchati tu.Mungu akubarki na uendelee kutukumbusha mengi zaidi

    ReplyDelete