Social Items

PropellerAds
MWANUME JIANDAE KUKUTANA NA TABIA HIZI KWA MWANAMKE UTAKAYE 
MPENDA 

Mwanaume anapoiingia katika ulimwengu wa mahusiano ya kimapenzi ni lazima mwanaume huyo atakutana na wanawake wenye tabia tofauti tofauti, ni miongoni mwa  tabia za wanawake walio wengi katika mahusianao ni pamoaja na:
Mwanamke asie na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke ambaye hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo makusudi huku akiwa ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema umuogope sana.
Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganisha watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.
Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupita kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kugeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.
Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.
Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Kwanza aina hii ya mwanamke niwakumuogopa sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.
 Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au laah! Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi ( Kukusaliti). Kwahiyo kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwan

MWANUME JIANDAE KUKUTANA NA TABIA HIZI KWA MWANAMKE UTAKAYE MPENDA 

Mapenzi ni kitu cha ajabu sana, watu kutoka koo, makabila, mataifa na wenye rangi tofauti hujikuta katika dimbwi zito la mpenzi ambalo wao wenyewe hawawezi kujizuia tena kamwe.

Hujikuta katika wakati ambao kila mmoja haoni kitu kingine cha thamani zaidi ya mpenzi wake. Huu ni wakati ambao si tu kuwa neno usaliti linakuwa halipo bali wapenzi hawahisi hata kama kuna maisha bila ya yule wampendaye.

Katika kipindi hiki hakuna lolote litakaloonekana ni kosa kwa yoyote. Hata ukipiga chafya mwenzako huona umeumi. Na atakusindikiza kwa pole mpenzi nikusaidieje. Utajibiwa ni chafya mpenzi asante. Kipindi hiki kila MTU humuona mwenzake anauzuri wa ajabu ambao haufananishwi na yoyote. Katika kipindi hiki ndio tunasema upofu umewatawala .

Usaliti ni hali , tendo, mwenendo, uamuzi wa kwenda kinyume na makubaliano yaliyowekwa miongoni mwa wapenzi wawili.

Usaliti ni jambo lenye maumivu yasiyovumilika hasa ikiwa ni jambo ambalo halikutarajiwa na mhusika.

Kutokana na maumivu yake kumekuwa na visa vingi vya kulipiza visasi, kujiua, kuuana n.k kunakotokana na maumivu ya usaliti.

Kutokana na hali hii basi utakuta wanawake wanajionyesha wazi wazi namna wameumizwa na usaliti huo kwa kulia ama wengine kujidhuru ama wengine kujiua . wengine kunywa pombe kupitia kiasi, wengine kufanya mapenzi ovyo na kuwaacha wanaokuwa nao ili ukilipiza kisasi tu .

Hata hivyo Leo tutaangalia Jinsi wanaume wanavyopokea hali ya kusalitiwa na Je wanaumia na kuonyesha maumivu yao?
Kwa nini  basi huishia kujiua na kujidhuru. Wengi wao kuwaumiza na kuingia katika makundi mabaya ?

Kwa nn basi wanaume huumia kwa muda mrefu kuliko wanawake ?

Wanaume si wepesi kusema yaliyowasibu.
Ukisikiliza vyombo vya habari au kusoma magazeti ni rahisi kukuta story ya mwanamke anayelalama baada ya mpenzi ,mchumba au mume au mume kutoka na mwanamke mwingine. Lakini ni nadra sana kukuta mwanaume akilalama! Si kwa kuwa hawaumizwi au hawana majeraha, bali ni sababu kwa wanaume inaonekana kama kujidhalilisha kusema hivyo.


Hawatamani hata rafiki zao wajue kilochotokea. Huishia kuumia peke yao, huishia kuhuzunika peke yao hiyo hupelekea kujenga majeraha makubwa moyoni.
Kuendelea kufuga hasira ambazo saa nyingine hupelekea wao kufanya maamuzi ya ajabu na yenye kustaajabisha kwa jamii.

Mwanaume hupenda kuendelea kuwa na nguvu juu ya jambo fulani siku zote
Ndiyo,kwa mwanaume kuwa na watu wanaomtii, wenye kumheshimu na kumsikiliza ni jambo linalompa faraja na kumfanya ajivunie. Mwanaume anapokuwa na mwanamke hupenda kuona huyo mwanamke akimnyenyekea, akimtii na kumsikiliza. Kwa taarifa yako mwanaume hapendi hata yule mwanamke asiyempenda awe wa kwanza kusema imetosha, au awe na mwanaume mwingine, inapotokea hayo humfanya mwanaume ajione amepungikiwa kitu, humfanya ahisi yeye si bora tena hapo ndipo tatizo linapoanzia.

Wanaume wana tabia ya kumuamini sana mwanamke wanayekuwa naye
Moja kati ya kazi ngumu kwa mwanamme ni kumfanya amwamini mtu mwingine kwa kiwango kikubwa, Inaweza kuchukua miaka mpaka kufikia hatua ya kumuamini mtu mwingine hasa mwanamke. Lakini inapotokea akafanya hivyo huamini jumla. Hatua ya kumuamini sana mwenza wake huleta madhara makubwa mbele ya safari. Tofauti na mwanamke ambaye siku zote anakuwa anawasha taa ya tahadhari na kujua inawezekana saa yoyote mpenzi wake atachepuka na inapotokea kweli mshtuko wake hauwezi kuwa sawa na mwanaume ambaye humwamini sana mwenza wake. Mwanamke anaweza kuzama kimapenzi au hata kuolewa na mwanaume asiye mwamini ni ngumu kwa mwanaume kufanya hivyo.

Sio rahisi kwa mwanaume kuhamisha upendo
Katika ulimwengu wanaume ndiyo wanaongoza kwa kuwa wasaliti kuna msemo unasema ‘every guy cheats’, ukweli tusioujua ni kuwa pamoja na kuwa wanaume hucheat zaidi kuliko wanawake ila wanafanya hivyo kwa sababu ya tamaa ya miili na nafsi zao hubaki kwa wenza wao wa kudumu.
Si rahisi kwa mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda na kuhamishia mapenzi hayo kwa mwanamke mwingine. Mwanamke anapokuwa mpweke Nna akatokea mtu ambaye akamtolea ule upweke anakuwa ameuwin moyo wake.

Usaliti umetokea ameamua alivyoamua, huo sio mwisho wa maisha kuna sababu nyingi za wewe kuendelea kuishi na kufurahia maisha. Pengine haya yanaweza kusaidia kukuamsha tena na kuona maisha yapo na hakuna sababu ya wewe kuumia. Tafadhali endelea kutembelea ukurasa wetu Kwa mada nyingine nzuri. Washirikishe na wenzako watembelee ukurasa huu pia. Karibu sana 

SALITI

Hii ni zawadi yangu kwako leo .

Je, wewe ni mtu ambaye unafanya jambo halafu baadaye  ukuulizwa kwa nini umelifanya ukawa na majibu mawili tu; ‘sijui’ au ‘si kina fulani ndo wamefanya’. Basi kuna majina mawili ambayo hawa watu huitwa mtaani, kama si bendera fuata upepo, basi ni boya (huwa linafuata maji yanapokwenda).

Yaani wewe mwenyewe huna sababu binafsi ya kufanya mambo unayofanya zaidi ya kuona wengine wamefanya ukafuata mkumbo tu. Ukiona mtu anafanya mambo dizaini hiyo, huyo hajitambui!

Tuulizane hapa leo kiroho safi tu; hivi unajitambua? Kama unadhani unajitambua endelea kujinoanoa hapa, ila ukiacha kusoma huu mchongo wewe ndo bado hujajitambua kabisa. Ngoja leo tupeane maujanja kuhusu kujitambua.

Kujitambua ni nini?

Basi hapo warembo mshashika vioo mnajiangalia, sio kujitambua sura, ni deep zaidi.

Ni kufahamu tabia zako, hisia zako, nguvu na udhaifu, jinsi unavyofikiri na kutatua mambo, ambavyo vyote kwa ujumla wake vinatengeneza ‘image’ yako ya jinsi unavyojichukulia na kuwachukulia wengine pia.

Kujitambua hutusaidia kufanya maamuzi sahihi ya jinsi ya kukabiliana na misukumo mbalimbali toka kwa marafiki zetu, ndugu, jamaa na mazingira yanayotuzunguka.

Dalili za upungufu wa kujiamini

Mtu asiyejiamini mara nyingi hushindwa kujitegemea kimaamuzi na kusubiri watu wengine wamuamulie. Hiyo ina maana huna maamuzi binafsi huna msimamo. Hiyo hupelekea kutoheshimika kwenye jamii inayokuzunguka. Na kwa maana hiyo basi hata mahusiano na watu huwa mabovu.

Jinsi ya kujitambua

Kujitambua ni ujuzi. Hii ina maana kuwa unatakiwa kujifunza jinsi ya kujitambua na kufanyia kazi ujuzi huu kila siku ili uweze kuwa mkali wao katika masuala ya kujitambua.

Kwa nini kujitambua ni muhimu?

• Ni tabia ambayo inasaidia kutatua changamoto za kimaisha.

• Kuweza kuelewana na watu.

• Unaweza kujenga mahusiano bora kati yako na familia na marafiki.

• Inasaidia kutatua matatizo ya kimahusianobadala ya kuweka chuki na kinyongo kwa watu, zzunaongea nao na kutatua migogoro.

• Moyo unakuwa na amani hata wakati wa matatizo makubwa, kwani unakuwa na uhakika wa jinsi ya kuweza kuyatatua.

• Unafukuzia mbali ‘stress’ zote zisizo kuwa na tija yoyote katika maisha yako.

• Unajijengea kujiamini na uwezo wa kuwapotezea kwa urahisi wale wote ambao wanajaribu kukuletea matatizo katika maisha yako.

Ili kujitambua inatakiwa:

1. Kuwa na maamuzi binafsi. Fanya unachojisikia kufanya pasipo na nia ya kuwaumiza wengine au kuvunja sheria lakini bila ya kufuata mkumbo wa wengine wanachokifanya. Mfano: Kama washkaji zako wanapanga kwenda sehemu, na wewe hujisikii kwenda usilazimishe kwenda na wala usione aibu kuwaambia ukweli.

2. Chukua muda kutafakari kuhusu maisha yako ulipotoka, hapo ulipo na unapotaka kuwa na njia gani zitakusaidia kuwa bora zaidi.

3. Kuwa muwazi katika mambo unayoyafanya.

4. Usipende kuhukumu watu haraka kutokana na vitu wanavyovifanya bila kujua ni nini kilichowasukuma kufanya wanachokifanya.

Kumbuka

Kujitambua ni ujuzi unaoweza kuupata kwa kujifunza na kuutendea kazi. Mtu anayejitambua hufanya maamuzi kwa matakwa binafsi na kwa sababu anazoweza kuzielezea. Jitambue.

Zawadi

Aisee hii nimeikuta huko soma ikusaidie kijana usiwe unapiga tu kelele wakati ni vocha tu teh.teh.. Huyu ni KIJANA MWENZENU AMEANDIKA HII

Amekuomba hela ya vocha unaanza kumtangaza eti yule mwanamke anapenda hela! Ndugu yangu Mungu anakuona, sasa kwanza hela gani ulizonazo mpaka useme kuwa atazipenda.

Hembu acha kutuaibisha wanaume wenzako angalau useme basi kakuomba umnunulie gari ndiyo kutokana na hali yenyewe tutasema kweli huyo kazidi. Lakini vocha, kaomba hela ya saluni ya nywele ambazo mwisho wa siku unaenda kuzivuruga wewe.
Kaomba hela abadilishe hata underwear maana anaona aibu kurudia kila siku tena kwaajili yako, Mama yake anaumwa hata nauli tu ya kwenda hospitali unaanza kumharibia sifa kuwa eti anapenda pesa.
Tena unajifanya kidume kabisa unasema “Asingekua anapenda pesa ningemuoa” Eti, nitamuoa asiyependa pesa, asiyeniomba fedha, ndugu yangu. Wewe sema tu umbahili au huna pesa basi tukuelewe moja kwa moja kuliko kumharibia binti wawatu sifa.

Tena mwingine unaenda kwake kila siku, kitanda kanunua mwenyewe, chumba analipia mwenyewe, jiko mwenyewe na kila kitu na bado unakula akiomba pesa unajifanya anapenda pesa. Wewe unafurahia kumwona anapendeza tu, tena usivyo n aibu unamsifia bebi umependeza gauni zuri nywele umesuka vizuri wakati haujagaramia hata kitu kimoja . Na wala hauna aibu na hilo unaona ni sawa tu. 

Labda nikuambie kitu wanaume wenzako wanaposema “huyu mwanamke anapenda pesa” hawamaanishi wameombwa vocha au pesa ya Pedi hapana, wameombwa pesa ya kiwanja na milioni moja ya Brazilian Hair. Vocha sio ela ya kupiga kelele Kwa mwanaume hata kidogo. Tubadilike basi tusiwafanye waonekane wanatamaa kumbe sisi ndio hatuelewieki.

Sipendi Kuombwa Hela

If you only know the value of your friend who is there  for you no matter what. you will love, care, and cherish him/ her for the rest of your life.

These friends are very rare to find and keep. And also it is very difficult to know them. They my not have a lot of money or big names. But they have a very big hearts. Big eyes and ears with a wide chest and shoulder to cry on. On my side if I find one I will cherish him or  her for the rest of my life

Friends