Social Items

PropellerAds

KISA CHA BABA MAMA NA BINTI YAO

MWANANGU HATA MIMI BABA YAKO SIJABADILIKA BALI NIMEZEEKA!
Binti mmoja alikua analia chumbani, alitoka kwa mume wake na kumfuata Mama yake, alikua anamuambia kua ndoa imemshinda hivyo anataka kuondoka. Mazungumzo yao yalikua kama ilfuatavyo.
BINTI; Mimi siwezi tena ndoa Mama, mwanaume kila siku ananipiga, kila siku anabadilisha wanawake kama nguo, juzi tu katembea na rafiki yangu yule ambaye alitusimamia katika harusi yetu.
MAMA; Vumilia mwanangu, utaacha wangapi, wanaume wote ndiyo walivyo, usiondoke kwenye ndoa eti kisa kipigo, yaani ndiyo umeolewa umuachie mwanamke mwenzako mume wako.
BINTI; lakini Mama nimechoka, ananipiga sana, hembu ona (akimuonysha makovu mgongoni) nimechoka bora niondoke nitafute maisha yangu.
MAMA; Usiondoke mwanangu, hata mimi na Baba yako tumepitia mengi, nimevumilia mengi, unafikiri ningetaka kuondoka nyie mngekua hivi?
BINTI; Kwani na wewe Baba alikua anakupiga? Hata yeye alikua na wanawake wengine?
MAMA; Mwanangu ndoa ina mambo mengi, Baba yako naye ni mwanaume, zamani alikua ananipiga, alikua anawanawake wengi, lakini leo wako wapi? Nilivumilia leo hii nina furaha, umeniona silii tena, hanipigi na hao wanawake si chochote mimi ndiyo kila kitu, vuumilia mwanangu, uvumilivu unalipa.
(Kabla binti hajajibu chochote mlango ulifunguliwa, Baba yake aliingia na kila mtu akabaki kimya.)
BABA; Acha kumjaza mtoto ujinga, mwanangu sikukusomesha ili uende kuvumilia mwanaume mjinga kama mimi Baba yako, nilikusomesha ili usije kuwa kama Mama yako. Mume wako hatabadilika, nawafahamu wanaume wa namna hiyo, mimi ni mmoja wapo, usipobadilika wewe yeye hawezi badilika.
MAMA; Mume wangu acha kumdanganya mtoto mbona wewe umebadilika na mimi nishahidi!
BABA; Wewe mwanamke sijui una akili gani? Hivi nimebadilika au nimezeeka, hivi unafikiri kwa uzee huu naweza kumudu kuchepuka?  Natamani sana lakini hizo nguvu ziko wapi? Unafikiri sikupigi kwakua nimebadilika, hivi kwa hali yangu kushuka kitandani tu shida nikikupiga wanao wakikuchukua nikabaki hapa mwenyewe si nitakufa?
MAMA; Kwahiyo uansema hujabadilika?
BABA; Mwanangu mwanaume habadiliki kwakua unavumilia ngumi na mateke, habadilikia kwakua unamchekea akitembea na rafiki zako, anabadilika ukijitambua na ukijua thamani yako! Mama yako anakudanganya hata yeye hakua mvumilivu, alikua hana kazi ya kufanya kumuingizia kipato kwangu alivumilia kwakua alikua hana pakwenda, alisharudi kwao Baba yake akamuambia hawezi mpokea mpaka nimpeleke na mimi nikakataa, alishanichoka na mimi sijabadilika nimechoka. Usisubiri wakwakoa akachoka, atakuja kukuua kwa ngumi au UKIMWI!
Baba huyo akatoka na kuondoka zake, alimaucha Binti na Mama yake wakiangaliana tu! Kama umemuelewa huyu Baba hongera sana .

No comments