Social Items

PropellerAds
Kuwa single kwa kuachika, kuachwa, kutokupata mwenza, kuumizwa ama kutokupenda tena. Kunawafanya watu wengi sana kubadilika na kuonekana watofauti katika jamii .
Kwa experience ni kwamba watu waliokaa single kwa muda mrefu ni wagumu sana kufanikiwa kwenye mapenzi (sisemi wote ila wengi sana), watu hawa ni wagumu sana kupendwa maana wanajiona wameshazoea sana ile hali ya kuwa wenyewe, kujitegemea, kujisimamia wenyewe na kufanya mambo yao pasipo mtu mwingine, wanajiona wanajitosheleza, ni ngumu na inahitaji upako wa ziada kumshawishi yeye kukuonyesha kwamba anakuhitaji wewe au unaumuhimu kwenye maisha yake
Hili pia linawafanya watu wengi wawaone kama hawako Sawa ila wao hujiona wako Sawa na wanakuwa na amani kabisa. Ni ukweli usiopingika kuwa kupenda tena kama mwanzo kwao ni ngumu ila wanaweza kupenda kwa taratibu sana.
Kundi hili huwa halipendi sana usumbufu na hupenda kujiweka pweke pweke sana. Ikitokea tu miadi yako itagusa mambo yake ya msingi ambayo angeyafanya kwa mustakabali wa maisha yake basi ujue miadi hiyo iko mbioni kivunjwa hata kama   kwako ni ya muhimu sana .
Wengi huwaona kama wanyimi (wako selfish) sana lakini ukweli ni kuwa wameshajenga wigo na ukuta wao kwa namna hiyo na haiwezekana uingie kirahisi rahisi tu, kwani hujiamini katika mengi wayafanyayo
Tusiwachukie tuwapende kwani ni sehemu ya maisha waliochagua kuishi na wanayafurahia kwa naman hiyo.
Inawezekana haoni thamani ya penzi tena , labda kwa sababu y kuumizwa ama kuachwa ama vyote. Ukimwona ukampenda nenda naye taratibu . kadri utakavyomwonyesha kupenda kujali kumhitaji mbegu ya upendo itakuwa ndani yake n ataanza tena kuona upendo. Usilazimishe nenda polepole, usiwe n haraka sana wanapenda n wakiweza kukupenda wanakupenda kweli.
Akifanikiwa kuingia kwenye mapenzi akadumu Huyo hudumu milele. Ila akianza kuona n  kuweka mashaka na kuona  taa za njano na nyekundu zikiwaka mmh ni ngumu kudumu naye. 
MPE mazingira ya kawaida sana ili aweze kuwa na amani thidi ya kile unachotaka kikue ndani yake. 
Hakikisha unamwelewa na kufahamu alipoumiziwa, jua haswa n nn kilimuumiza. Anza kwa kumsoma hapo usirudie yale yaliyomuumiza. Ili umjenge tena. Hakikisha unamnyanyua kutokea hapo atalifurahia pendo hilo.
Wanaume ama wanawake wote huumizwa kwa namna moja ama nyingine. Jitahidi kurejesha kendo tena kwa MTU aliyeumia, aliyekata tamaa ya kupenda, asiye n hamu ya maisha hayo tena. 
Ni rahisi sana Wewe anza tu kujua n wapi palileta shida usiparudie. 

Jenga ukaribu naye.
Msaidie anapokuwa n uhitaji. 
Mshike mkono pale anapojikwaa ili ainuke tena. 
MPE faraja anapohitaji taratibu atapona na atakuwa sawa tena. 
Nawapenda . endelea kibaki hapa hapa www.monicamoshiro.com uendelee kupata mengi mazuri zaid. Usiache kutoa maoni yako.

Kuwa single kwa muda mrefu

 TUJIREKEBISHE HAPA

Wakati mwingine dada zangu huwa mnachekesha na sijui nani kawaloga kwakua mnmajitengenezea mambo yenu huko kichwani na kutaka wanaume kuyafuata. Kwanza mnajua kuwa wanaume wengi ni waongo, mnajua kuwa ili kuleta amani mwanaume anaweza kukuambia kitu chochote kile ili tu upunguze kelele! Kwamba ili kujua kuwa mwanaume wako anamaanisha kile anachokiongea au anakudanganya ni kuangalia matendo yake, kwamba kama anakuambia kuwa anakupenda lakini kila sikua nakupiga basi anakudanganya!

Kama anakuambia kuwa nitakuoa lakini hata kujitambulisha kwenu ni shida basi jua kuwa ni muongo! Mnatakiwa mjue hivyo na kama ulikua hujui basi huo ndiyo ukweli, ukiwa na mwanaume yeyote kamwe, narudia kweme usisikilize maneno yake, angalia matendo yake, kile kitu mwanaume anachokuonyesha kimatendo ndiyo hicho hicho kilichopo moyoni mwake! Kama anakunyanyasa, anakusaliti, anakupiga na hataki kuja kwenu huyo mtu hakupendi na acha kujidanganya kuwa sijui atabdilika sijui na mautumbo mengine mengi!

Sasa tuachane na hilo, kuna hili la wadada ambao akishaishi na mwanaume muda mrefu anaanza kulazimishia kuwa unakuja kwetu lini kujitambulisha. Hapa sizungumzii wale wapenzi tu, hapana nazungumzia wale viherehere wanaokusanya nguo zote na kuhamia kwa mwanaume. Sasa dada yangu aje kujitambulisha kwani alikuambia anataka kujitambulisha! Hivi unafikiri kuishi na mwanaume nyumba moja mwaka ndiyo atakuoa au unadhani anataka kujitambulisha. Kwanza hilo swali ulitakiwa uulize kabla ya kuhamia kwake na si baada, angekua anataka kukuoa angekuoa ukiwa kwenu lakini wewe ushajiozesha ndiyo unauliza.

Kuna wale wengine sasa sijui ni kama hamjui siku zenu lakini ghafla unabebe mimba ya mwanaume hajakuoa iwe kakuambia au bahati mbaya lakini unabeba kisha unaanza kuuliza lini unakuja kwetu! Dada yangu unachekesha, aje kwenu kufanya nini? Angekua anataka kuja kwenu angekwisha kuja kipindi huna mimna kama alikua na nia hiyo lakini mimba haiwezi kumfanya mwanaume kukuoa ndiyo  maana kuna single mother kibao mtaani! Ukibeba mimba ni yako lakini sio uanze kusumbua watu na kulazimisha wakajitambulishe wakati hata hawakua na mpango wa kuoa.

Wimbi la single parent hasa single mothers limeongezeka kwa Kasi kubwa Sana hasa Kwa mabinti wadogo wadogo na hili linatokea mara nyingi Kwa kukosa kujitambua tu n kuona kama kubeba mimba ndio suluhisho la kupata ndoa . Kwa nn huwa munapata shida Sana na hili Jambo la ndoa ? Nani alisema ukitulia n kuwa n msimamo wako ndoa hauipati ama Nani alisema usipoolewa Hakuna maisha .? Maisha n maisha yapo inategemea unayaangaliaje tu. SASA unajikuta una watoto wa NNE huna kipato unaanza kupata shida ya kwenda kutafta kesi za matunzo Baraza za usulihishi Kwa nn mumefika huko  Kwa sababu mulikosa maamuzi n msimamo.

Usijiachie kiasi hicho. Kukuambia nakupenda hajasema tuzae hajasema tuoane hajasema wewe n mke . Na hata akisema ujue kabisa kuwa n lazima matendo na taratibu zifuatwe .

Wapo waoamua kuwa single parent Hao siwazungumzii kabisa wala hawahusiki hapa. Hapa Niko n wale wa Bahati mbaya ama wale wa mimba ndoa hahah Hao ndio ninaosema nao . Tujitambue tu . Mwanamke ukijitambua Hakuna kulia Lia bure

Mwanaume anakuambia anakupenda Sana Ila hawezi hata kujishughulisha n wewe Kwa lolote Ila akishafika wakati ule anahitaji mwili wako ndio maneno matamu yanamtoka n sifa kemkem . Si ujiongeze yeye anakupenda tu akiwa n uhitaji wa tendo basi . SASA mwenzangu mukishaona Hilo wewe unajirahisi tu unaufungua na moyo wako alfu unaishia kuumia tu .. sijui n Nani amewaloga aiseee ACHA kubeba  miili ya watu ACHA kuwa dampo la kupokea tu kisa umeambiwa wewe n mzuri sijui mrembo sifa hizi hazukusaidiia kitu n lazima ujue kungamua lililo kweli n la uongo

ACHA kujipa majibu ya maswali n kujipa kile unataka kusikia tu. Usitake kusikia mazuri tu kutoka Kwa mwanaume ama mwanamke wako yeye sio Malaika n mtu huyo anayo mazuri n mabaya pia. Wewe umekuwa wa kutaka kusikia tu mazuri n kujipa majibu yako. Kwa nn lakini Kwa nn unajiambia atajua mahitaji yako . SEMA moja Kwa moja nahitaji ela ya kitu Fulani sio unafikiria tu kuwa huyu atajua Bila wew kumwmabia ataota SASA . Kwan yeye n Malaika ndio ajue tu Kila kitu. Wanawake wengi wamekua na hii tabia kuwa mbona sifanyiwi hili ama lile nakuukiza tu anajuaje kuwa unataka Hilo Bila wewe kusema . Mweleze aelewe mwambie alfu uone kama hafanyi, usijifanye atajua tu Nani kakuambia atajua tu.

TUJIREKEBISHE HAPA

Mwanaume  ni kiumbe anayehutaji kutawala n kuwa mfalme hasa anapokuwa katika himaya yake . Huwa anajitahidi kuhakikisha anaonekana kuwa yeye ndii mtawala n kiongozi mahali hapo.

Kutokana n hali hiyo wengi wa wanaume wanashindwa kuelewa njia nzuri ya kutawala iwe kwenye familia, Kazi ,ama shughuli nyingine yoyote .

Hili linawafanya wanakuwa wababe San hata katika eneo lisilohitaji ubabe n nguvu za ziada utamkuta mwanaune yeye ndiye Mume , ameoa ana mke na watoto Ila kila siku  anapiga mke, ananyanyasa watoto, anamnyanyasa mke na kila wakati anamalizia kauli zake na maneno kama, tutajua mwanaume ni nani humu ndani, mimi ndiyo mwanaume nishasema, kauli yangu ndiyo ya mwisho, nimesema sitaki mimi ndiyo mwanaume basi jua huyo ana matatizo.

Mwanaume anaamua kufanya maamauzi yake tu Bila kumshurikisha mke wake .. Kwa kisingizio cha kuwa yeye n mwanaume unanunua eneo, unaacha Kazi, unaamua kuoa Kimya Kimya, yaana haya yote na mengine yanakuonyesha jinis gani  usivyo kiongozi n usivyo jua sehemu sahihi ukiyonayo katika familia yako. 

Mwanaume kiongozi ,mtawala hajui kupiga mke Bali hujua namna y kuelekeza. Kumbuka huu n ubavu wako unapoupiga n kuunyanyasa huyo n wewe n sio mwingine kwa nn basi ujitese mwenyewe... Si n wewe uliyesema huyu n mfupa katika mfupa wangu m nyama katika nyama yangu .... Ama umesahau hilo.

Mwanaume anweza kumwache mkewe anatembea kwa miguu n usafiri anao na akaona Sawa tu huyu hayuko kamili

Mwanaume anayeweza piga mwanamke mwenye mimba eti amekuudhi huyu naye sio Sawa tabia hii n mbaya . Hata kama kakosea tazama Yule mtoto tumboni mwache . Watu wazima hawaonyani kwa vipigo Ila huelezana tu na wakaelewa vyema kabisa

Kuna wakati maudhi yanatokea katika mahusiano lakin hiyo sio sababu ya kubweka ovyo ama kupiga ovyo ... Mwanaune anakuwa n kisirani tu Kwa sababu mkeo kakuzidi kipato hutoi Tena hata hela ya matumizi humudumii Kwa lolote uko unapiga tu kelele na matusi ya hapa n pale

Sasa kaka zangu inakuwaje unapigaaa wee kama unapiga ngoma. Tena unashindwa kabisa kumwomyesha mkeo mapenzi n mahaba yote eti kisa wew n baba n unajidanganya ukimwomyesha atakudharau.. Acha kabisa mwomyeshe akiwa hai huyo ndio mkeo n ndiye mama wa watoto wako 

Umepewa huyo kuwa mshauri wako . Wakati unamuoa hukuona kama anamapungufu? Kwa nn basi kumtukana mbele za watu n watoto kuwa anaakili fupi, hajasoma, mshamba, hafai,moumbavu, mjinga. Mara haendani na Wewe kiakili kwani hukuwaona hao wanaoendana n wewe wakati unamuoa. Wewe  uliona anakufaa Kwa Kila idar leo imekuwaje ? Leo nini kimetokea ? Mbona unaanza kujibagua kuwa huyu sio saizi yangu 😁😁😁 Nataman waanaume wajue namna munawaumiza wake zenu kwa maneno hayo. Kama unaona yeye hakuwa sawa n wew kielimu mwendeleze basi MKE ANASOMESHWA IKIBIDI . kama unaona havai unavyotaka MNUNULIE UNAVYOVITAKA atavaa atakuwa sawa n class unayoitaka . Wewe umeshamuoa MBADILISHE MTENGENEZE utakavyo Wewe na atakuwa.

Kuna mambo ama Kuna kasoro , ndogo ndogo wanazokuwa Nazo wanaume n hizi huwafanya kuwa watu wa hasira, kisirani ,gubu lisilo la msingi mfano  inawezekana hahudumii vizuri familia yeye n kukoroma tu matumizi hakuna ukiuliza ugomvi, kitandani shughulia yake ni ya mashaka kwa sababu ya stress n lishe duni, hajiamini uwezo wake wa kufikiri au ana  kakasoro kengine . Kasoro hizi zinamfanya atumie nguvu nyingi zisizo n msingi badala ya kurekebisha tatizo yeye anaamua kutumia nguvu na kuharibu zaid.kwa kupiga watoto hivyo kugomba bila sababu n mke akihoji kitu ndio shida zaidi.

Mwanaume wa aina hiyo  ni sawa na gari bovu kila sehemu likipita nilazima lipige kelele ili kushairia kuwa linapita, watu wageuke walione. Au tuseme ni kama Mbwa muoga, anabweka sana ili watu wajue kuwa yeye ni Mbwa si paka! Kwani nini kupiga, matusi kwa nn gubu kwa nini .... n.k haya  hayakukufanyi uwe mwanaune kiongozi kamili. 

Mwanaume kamili anayajiamini na kujua majukumu yake hana haja ya kusema yeye ndiyo mwanaume," (MIMI NDIO BABA HAPA) ,"  bali yeye ni kama gari jipya, likipita kila mtu anageuka hata kama limesimama halitoi mngurumu kila mtu lazima ageuke. Ni kama mbwa mkali habweki lakini ukimuona tu utapita mbali kwakua hahitaji sauti kujitambulisha.


Wacha leo nikuambie kitu . Wanaume wote n wapole Sana wasikivu Sana n wana utu Sana Hawa n wale wanaume wanaojijua kuwa wao wanamjukumu gani hapa duniani. Wanaojijua kuwa wao n viongozi. Wanaojua kuwa mwanamke ametoka kwenye ubavu wake hivyo hawana hata ya kujiumiza wenyewe.

Hata hivyo  . Wanaume wagomvi wapo wanaojishtukia Kwa Kila kitu wapo. Tena wengi Sana .hawa hata utende jema gani kwao n baya Lakin unaweza kumbadilika n kuwa mtu mwema n kiongozi kama tu atakuwa tayari lwa hilo. upendo na kujali sana kunaweza mbadilisha akiwa tayari.

Najua Kabisa kila mmoja ana mapungufu take basi   usiyaendekeze n mapungufu ya  mwenzako yasiwe fimbo ya kumuumiza mwingine . yatumie kutengeneza upendo. 

MWANAUME KIONGOZI

Katika maisha haya . hasa maisha ya mahusiano unapaswa kujichunguza sana na kuwa n msimamo juu ya maamuzi unayoyafanya .
Kumbuka sio kila anachofanya rafiki yako n wewe ufanye kama yeye , na wala sio kila maamuzi anayoamua na wewe uamue kama yeye 

Kumbuka pia Sio Kila EX Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha! Wengine Huomba Kurudi Ili Wakutesti Tu Jinsi Ulivyo Mbulula,Jinsi Usivyo Na Msimamo Na Jinsi Ulivyo CHEAP Na Huna Misimamo Wala Future. Wengi huishia kulia n kulaumu tu. Nikuulize kama aliondoka sasa anatafta nn ? Kama alikusaliti unafikiria ataacha kwa sasa? Kama alikuone haufai unafikiria sasa ndio utamfaa? Jifunze basi kuwa expensive kidg tu .
.
Jitu Mmeachana Miezi 6,Leo Linakutesti Lirudishe Majeshi,Na Wewe Ulivyo Kiazi,Upo-Upo Tu,Ina Maana Miezi Yote Hii Ulikuwa Umeganda Unasubiria Rehema Zake Ama?? Kurudia Matapishi Ya EX Ukitegemea Amebadilika Ni Sawa Na Kupika Sufuria La Makande Kwa Mshumaa,Utaambulia Masizi Tu.. Hahaha wacha nicheke mie hivi unajua kuwa amekwenda huko anarudi na anajua udhaifu wako anajua uongo gani akikuambia wewe uko hoi hahaha tena unajidanganya amebadilika waaapi wewe .. Uliona wapi ngozi inabadilika hata wapaka mikorogo watakuambia wakiacha huwa inarudi ndio ilivyo tabia n kama ngozi tu
.
Kipi Kipya Kakiona Kwako Hadi Arudi??Nini Kilimshinda Huko Nyuma Ambacho Leo Anakiweza Anataka Kurudi??
.
KUWA NA MSIMAMO,Ukisema Its Over Umaanishe,Sio Unakuwa Na Hisia Zinapepea Tu Kama Bendera Ya Katibu Kata Wa Kishumundu… hahaha Dada au kaka unaumia wewe unayeendekeza upuuzi huu yeye atakutumia na ataondoka vile vile

Huwezi Kusoma Degree Ya Law Halafu U-Apply Kazi Ya Chief Accountant Wa Bodi Ya Pamba…Kila Siku Utasingizia Balance Sheet Haina Jurisprudence..Lawyers
Mmenielewa! Acha Kudate Watu Wasiojielewa,Usidate Kwa Sababu uko Lonely,Usiwe Desperate kuingia Mahusiano kwa Sababu rafiki zako wanakusimulia walivyopelekwa Ruwenzori Waterfalls.. Si umwage maji juu uangalie yanavyoanguka n wewe ufurahie kuliko kuumiza moyo wako kila siku n kila Mara .
.
Ingia Kwenye Mahusiano Pale Moyo Wako Ukiwa Tayari Na Mtu uliyemfia Kihisia na Amekuwa Approved Na Veins,Auricles,Na Aorta Za Moyo Wako Kwamba He/She Is Really The One.. Unadate Na Mtu ambaye Mustakabali Wake Mwenyewe Haujui,Ukimuuliza Anataka Kuwa aapi ndani ya Miaka 5 Ijayo Anakwambia Mungu Anajua Dont Worry,Halafu BBM Na Instagram Unajiita Baby Ake Mie Iam In Love..
Utaishia Kufua Boxer tu! Mbwa Kamwe hashughuliki ba Kesi za Paka Kufungiwa Kabatini.Date The Right Person,With Right Reasons,In A Right Time Uone Kama Mapenzi Hayapo…


Na KUELEZA LEO MAPENZ YAPO HAYAWAI WALA HAYACHELEWI YAPO JARIBU KUUJUA WAKATI JARIBU KUWA N MSIMAMO ALAFU UTAONA KAMA YAPO AMA LA .. YANGU N HAYO TU KWA LEO 😀😀😀


KUWA NA MSIMAMO


Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule. Lakini, kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, mwandishi wako Dk. Khamis Hassan anajaribu kutueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.


1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo:


Wanawake ambao hufika kilele (orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana. Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee. Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.


2. Huongeza ukakamavu wa mifupa:


Wanawake waliokoma kupata hedhi (menopausal women) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya  oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis.


3. Hupunguza msongo wa mawazo:


Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili kupumzika, muscle relaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vya prostaglandins katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema.


4. Hupunguza maumivu:


Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post menopausal syndrome symptom).


5. Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume:


Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.


6. Huongeza uwezo wa kunusa:


Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo (brain stem cells) kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa  na kutambua harufu (brain olfactory bulb).


7. Hupunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema:


Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200 calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi.


 8. Huongeza kinga ya mwili:


Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.


9. Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke:


Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa.


10. Kudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida:


Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa.


11. Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini:
Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.


12. Kuongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles): Na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke (vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na  maambukizi katika njia cha mkojo (Urinary Tract Infection).


13. Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini:


Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali mwilini.


14. Huongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako:


Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote.


15. Husaidia kuishi kwa muda mrefu:


Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele.  DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.


16. Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.


17. Uongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba: Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku nne. 


TENDO LA KUJAMIIANA

WEKA MIPAKA KWA KATIKA MAISHA YAKO  NA KUJENGA WIGO

Maana nyepesi ya mpaka ni mahali ambapo ni kikomo cha kitu na kingine, mfano nchi, kiwanja , shamba nk vina tenganishwa na mpaka. Wakati wigo ni ukingo, unaweza kuwa wa ukuta, nyavu, miti, nk hutumika kuzuia au kufanya watu wasiingie kirahisi katika eneo lilozungushiwa huo wigo. Na mara nyingi wigo hujengwa au kuwekwa sambamba na mpaka wa eneo husika.

Hivyo basi katika maisha yetu ya kila siku hatuna budi kuweka mpaka, sio kila mtu anatakiwa kuwa karibu na wewe, sio kila mazingira ni lazima uende, sio kila jambo unatakiwa kufanya na ili uweze kuwa hivyo ni lazima ujiwekee mpaka na umalizie kwa kujengea wigo.

Tena ikiwezekana weka wigo wa ukuta ukiambatana na umeme. Kuna mambo yametuumiza sababu tu tunaingilika kirahisi, kuna watu wametutesa sababu walipokuja kwako hawakuona wigo wala kukuta mpaka.

Hivyo wakakufanya chochote walichotaka halafu ukaanza kuwalaumu kwa uzembe wako wa kutoweka mpaka na kujijengea ukuta.

Unaonaje ukajiwekea mpaka kwamba saa nne usiku itanikuta nyumbani kwangu kama unakwako, au ukajiwekea mpaka kwamba saa moja itanikuta nyumbani kama ni kwa wazazi. Najua kuna dharula maana hamchelewi kuanza kusema mwalimu nawezaje kuwa na mpaka kama huo.

Kuna watu wamejiwekea mipaka hadi vitu vya kuangalia na kusoma, na imewasaidia sana. Wewe kila mtu anakuzoea kirahisi rahisi tu, umejirahisha wee huna hata mpaka. Umeshindwa kujimiliki sababu kama huna mpaka inamaana huna shamba, huna kiwanja yaani kwa lugha nyepesi humiliki kitu. Sasa kama huna mpaka yaani wewe hujimiliki na utasumbuliwa sana na kuishia kulalamika.

Weka mipka yako katika mambo pia ya kufanya ili uweze kufikia malengo yako kama hauna wigo ambao utakuwezesha kufikia malengo yako basi n taabu kuona mafanikio

Weka mipaka katika matumizi yako ya fedha au kipato chako chote unachokipat sio kila ela inayoingia inatumika bila hata mpangilio mzuri na mwisho wa siku namanza kulaumu na kusema ooh kazi fulani haifai ooh biashara hii n ngumu mbona wenzako wanatoka wewe hautoki kwa sababu hauna mipaka na hauna wigo

Mwaka unaisha vibaya kwako moja ya kosa ulilofanya ni kutojua mipaka yako na kujenga wigo. Hivyo umejikuta kila mahali unaenda,kila watu unashirikiana nao, kila kitu unasoma hauna mipaka.

Unapomaliza mwaka usikubali kuanza mwaka bila ya kuweka mpaka na kujenga wigo.
Karibu sana
Unaweza ku share na wenzako kama umeipenda .
Pia like page yangu ujifunze zaidi page yangu na Monica Moshiro  karibu sanaWEKA MIPAKA KWA KATIKA MAISHA YAKO  NA KUJENGA WIGO

WEKA MIPAKA KWA KATIKA MAISHA YAKO  NA KUJENGA WIGO
Maana nyepesi ya mpaka ni mahali ambapo ni kikomo cha kitu na kingine, mfano nchi, kiwanja , shamba nk vina tenganishwa na mpaka. Wakati wigo ni ukingo, unaweza kuwa wa ukuta, nyavu, miti, nk hutumika kuzuia au kufanya watu wasiingie kirahisi katika eneo lililozungushiwa huo wigo. Na mara nyingi wigo hujengwa au kuwekwa sambamba na mpaka wa eneo husika.
Hivyo basi katika maisha yetu ya kila siku hatuna budi kuweka mpaka, sio kila mtu anatakiwa kuwa karibu na wewe, sio kila mazingira ni lazima uende, sio kila jambo unatakiwa kufanya na ili uweze kuwa hivyo ni lazima ujiwekee mpaka na umalizie kwa kujengea wigo.
Tena ikiwezekana weka wigo wa ukuta ukiambatana na umeme. Kuna mambo yametuumiza sababu tu tunaingilika kirahisi, kuna watu wametutesa sababu walipokuja kwako hawakuona wigo wala kukuta mpaka.
Hivyo wakakufanya chochote walichotaka halafu ukaanza kuwalaumu kwa uzembe wako wa kutoweka mpaka na kujijengea ukuta.
Unaonaje ukajiwekea mpaka kwamba saa nne usiku itanikuta nyumbani kwangu kama unakwako, au ukajiwekea mpaka kwamba saa moja itanikuta nyumbani kama ni kwa wazazi. Najua kuna dharula maana hamchelewi kuanza kusema mwalimu nawezaje kuwa na mpaka kama huo.
Kuna watu wamejiwekea mipaka hadi vitu vya kuangalia na kusoma, na imewasaidia sana. Wewe kila mtu anakuzoea kirahisi rahisi tu, umejirahisha wee huna hata mpaka. Umeshindwa kujimiliki sababu kama huna mpaka inamaana huna shamba, huna kiwanja yaani kwa lugha nyepesi humiliki kitu. Sasa kama huna mpaka yaani wewe hujimiliki na utasumbuliwa sana na kuishia kulalamika.
Weka mipka yako katika mambo pia ya kufanya ili uweze kufikia malengo yako kama hauna wigo ambao utakuwezesha kufikia malengo yako basi n taabu kuona mafanikio
Weka mipaka katika matumizi yako ya fedha au kipato chako chote unachokipat sio kila ela inayoingia inatumika bila hata mpangilio mzuri na mwisho wa siku namanza kulaumu na kusema ooh kazi fulani haifai, ooh biashara hii ni ngumu , mbona wenzako wanatoka wewe hautoki ?Kwa sababu hauna mipaka na hauna wigo

Mwaka unaisha vibaya kwako moja ya kosa ulilofanya ni kutojua mipaka yako na kujenga wigo. Hivyo umejikuta kila mahali unaenda,kila watu unashirikiana nao, kila kitu unasoma hauna mipaka.
Unapomaliza mwaka usikubali kuanza mwaka bila ya kuweka mpaka na kujenga wigo.
Karibu sana
Unaweza ku share na wenzako kama umeipenda .
Pia like page yangu ujifunze zaidi page yangu na Monica Moshiro  karibu sana

WEKA MIPAKA KWA KATIKA MAISHA YAKO  NA KUJENGA WIGO

Mabadiliko katika mapenzi ni kitu cha kawaida sana, wakati mwingine mtu anahitaji muda wa peke yake, muda wa kutafakari mambo. Lakini kuna mambo mengine yakitokea unapaswa kuamka na kujua kua kitu.

Mara nyingi wanawake ni vipofu katika mabadiliko, wanaachwa na kuonyeshwa dalili zote za kuachwa  lakini bado wanang’angania hawaoni. 

Zifuatazo ni dalili kumi kuwa mwanaume wako hakutaki tena kashakuchoka na anakaribia kukuacha.
(1) Anawasiliana, anatamani na kuongea kimahaba na wanawake wengine mbele yako. Wala hajli upo, hajali kuwa anakuumiza, hajali kama unahisia, atawasilina na wanawake wengine, ataongea nao na kuongea maneno ya kukuumiza huku akikudharau mbele yao. Dada Unaachwa!

(2) Hakuchukulii siriasi tena; Yaani unaweza kuongea kitu wala hajali, mnaahadi hatokei na wala haombi msamaha, kuna kitu cha muhimu kinachokuhusu wewe wala hajali na haumizi kichwa, ukiongea hakuchukulii siriasi atakebehi na kukashifu kila unachoongea. Dada Unaachwa!

(3) Hakupigii tena simu wala kujibu meseji zako; Zamani ukibeep tu anapiga, lakini sasa wala hata hajali na ukipiga atakuambia nitakucheki ila ndiyo nitolee. Meseji ndiyo hajibu, yuko online au kwenye group, anacomment post ila wewe wala nikama vile haupo. Dada Unaachwa!

(4) Hakuonyeshi Tena Mahaba; Mambo ya kushikana mikono kama zamani hakuna, hataki hata kuongozana na wewe na wala kukushika sehemu lizokua anakushika awali, anakukwepa kwepa na mbele ya marafiki anajifanya kama vile si mtu wake. Kama alikua anafanya hayo mambo awali na sasa hafanyi… Dada unaachwa!

(5) Hataki tena kufanya mapenzi na wewe; Yaani imekua kama adhabu, mnaonana lakini wala hakutaki tena. Zamani alikua akikuona tu mziki wake unchanganyikiwa ila sasa ni kama unalazimisha. Hata kama ukiomba mechi ukifika hakuna rommnce wala kushikana kama analima vile kanyaga twende anakucha anaendelea na mambo yake. Dada Unaachwa!

(6) Anakuambia nataka kuwa peke yake “More Space” Kuna mambo anafikiria msionana. Mkipanga anakuambia atakutafuta na wiki inaisha hakutafuti. Dada kama una mwezi hujaonana na mpenzi wako mko sehemu moja anakupiga chenga wewe ndiyo ushaahwa. Mwanaume anamkwepa mwanamke akiwa na mwingine anampa huduma zote na si vinginevyo hivyo kama anataka space Dada Unaachwa!

(7) Hataki kuongelea tena mambo ya mapenzi; Zamani mlikua mkikaa kidogo anazungumzia maisha, watoto, sijui mapenzi yenu, mahusiano yenu na mahaba. Ila sasa wala hataki, ukiongelea hayo mambo anabadilisha mada, kukasirika na hata kuongea. Dada unaachwa!

(8) Hakusifii tena; Kuna wale wanaume ambao hata hawana hayo mambo, ila kama alikua anajua umevaa nguo mpya, umesuka ana kusifia umefanya kitu kizuri anakusifia ila sasa hata ukipendeza vipi hasifii ni kama vile hata hakuoni na hata ukimuambia wala hajali anajifanya yuko bize na mambo yake. Dada Unaachwa!

(9) Hakuheshimu tena; Zamani alikua akikuheshimu wewe kama mwanamke, anaheshimu kazi yako na ndugu zako, lakini sasa wala hajali, anakudharau anaweza kukudhalilisha mbele za watu na asijali, akakuona unadhalilika na wala hajali na kila wakati ni kutafuta neno hata moja la kukuudhi. Dada Unaachwa!

(10) Ameacha kuongele amambo ya ndoa: Ndiyo kuna ambao wala hawakua wakizungumzia hayo awali achana na hao. Ila kuna yule ambaye kila siku alikua ni namna akikuoa, namna sijui mkifanya hivi, mipango yake yote ilikua inakuhusiha na wewe.
Ila sasa hazungumzii tena mambo ya ndoa, yaani ukigusa hayo anakasirika na hata kukutukana. Au utasikia anasema mimi suala la ndoa sasa hivi bado, nataka nijinge kwanza, siwezi kuoa mpaka lini, sijui nataka mwanamke wa namna flani wakati upo na vitu kama hivyo. Dada ukiona hivyo jua Unaachwa.

Nimalizie kwa kusema kuwa hizi ni dalili tu kuwa huyu mtu kakuchoka na anataka kukuacha au kichwani kwake ashakuacha na ana mtu mwingine. Sasa kama anakufanyia yote haya wewe ushaachwa kabisa na ni wakati wakuwaza maisha mapya.

Lakini si wakati wa kukata tamaa, niwakati wa kuanza kujipenda na kujifanyia mambo yote ambayo unaona yatakupafuraha. Kuacha kujipendekeza na kumsujudia na kuanza kujipenda wewe kwa kujifanyia mambo yanayokupa furaha. 

DALILI ZINAZOONYESHA YAKUWA MWANAUME ULIYENAYE ANAKARIBIA KUKUACHA/ASHAKUCHOKA

EPUKA HAYA NDOA YAKO IWE YA AMANI
Yapo mambo mbalimbali unapaswa kuyaepuka sana ili kufanya ndoa yako ikae Sawa na istawi sana sana. Twende pamoja:
1.KUTOKUHESHIMIANA.
Si vizuri kumtamkia maneno mabaya mwenzi wako mbele za watu.
Mke au mume anahitaji kuheshimiwa, kupewa asante, kuwa appreciated na zaidi kumsifia mbele za watu na sivinginevyo.
Kuongea mambo mazuri kwa mke au mume wako mbele za watu ni muhimu sana.
Wapo wanaume hutukana wake zao mbele za watu na wapo wanawake hujibu mbovu waume zao hata mbele za watu au wageni. Kama kuna kitu amekuudhi kwa nini usisubiri mkaongee chumbani mkiwa wawili? Hakuna ulazima wa kumdhalilisha mbele za watu kiasi hicho. Subiria waondoke mubaki peke yenu muyamalize kwa upendo tu.

2. KUTOSIKILIZA MMOJA AKIONGEA.
Hii inajumuisha kuwa na mawazo ya mbali wakati mume au mke anaongea, yeye anaongea wewe unaendelea kuangalia TV, Unaendelea kusoma gazeti, unaendelea kusoma kitabu, Unaisikiliza laptop kuliko mume wako au mke wako.
Pia hii inajumuisha kuwa mbali kimwili (body language) wakati mwenzako anaongea, wapo wanandoa ambao hata mwenzake hajamaliza kuongea tayari anadakiwa kwamba najua ulichokuwa unataka kusema, pia wapo ambao hata ukiuliza swali yupo kimywa, mbaya zaidi ni pale unapoona na kuhisi mwenzako ana tatizo lakini ukimuuliza anabaki kimya au anakwambia hakuna tatizo, Inaumiza sana hasa kwa wenzetu wanawake ambao asilimia kubwa ya wanaishi kwa hisia, na kuumiza hisia zao ni kitendo kibaya sana, ni vitu vidogo lakini ni muhimu kuliko unavyodhani.

3. KUKOSA MAHABA.
Ukiacha mke wako au mume wako anahangaika na kutoridhishwa kimapenzi maana yake unachimba shimo ambalo ukijifukia utatokea jehanam, na kama unaona umepoteza interest na sex fanya kila njia kupata ushauri na msaada ili urudi kwenye mstari.
Matatizo mengi ya ndoa zinazokufa huanza kwa ugonjwa wa kutoridhishwa kimahaba na mume au mke.
Kumbuka ndoto za watu wengi kuoana ni kupata mtu atakayemtosheleza kimapenzi.

4. KUJIONA SAHIHI MARA ZOTE.
Hii inajumuisha wewe kuwa ndo msemaji na muelimishaji wa mke wako au mume wako, yaani wewe ndo unajua kila kitu, upo sahihi siku zote, au bila neno lako la mwisho basi information haijakamilika.
Siku zingine kubali kwamba umekosea au huna jibu, hakuna mtu anaweza kufurahia kuwa na mtu ambaye siku zote yeye ndo yupo sahihi labda kama unaishi na mtu mwenye mtindio wa akili.

5. KUTOKUFANYA KILE UNASEMA.
Siku zote Imani bila matendo imekufa na Imani ni matendo, “Actions do speak louder than words”. Ukisema utafanya kitu Fulani, fanya.
Wanawake ni viumbe ambao hutunza sana ahadi tunazowapa, hivyo usiahidi kitu ambacho huwezi kufanya, kwani mwenzio anaandika kwenye ubongo wake siku akija kukutolea mahesabu ya ahadi hewa umefanya utaipata fresh, pia na wanaume (si wote) kwa ahadi hewa hatujambo, tujifunze kufanya kila tunachosema.
Tusitoe ahadi tamu kumbe hewa, inaumiza sana.

6. UTANI UNAOUMIZA.
Kama mwenzio anakwambia utani wako unamuumiza achana nao, kuna utani mzuri lakini kuna wakati mnaweza kufikishana pabaya na lazima uwe makini kusoma saikolojia za mwenzi wako, kuna wengine anaweza kukutania wewe usikwazike, na utani huohuo ukimrudishia yeye anakwazika so be very careful usimuumize mwenzako.

7. KUTOKUWA MWAMINIFU.
Kudanganya na kuwa na siri zako binafsi katika mahusiano huweza kujenga wawili kuwa mbali na kutokuaminiana.
Hata kama kunaumbali hakikisha unajenga uaminifu
Mwenzako akikuamini ukaona hakufuatilii isiwe tiketi ya kukosa uaminifu . utakupoteza sana jifunze kuwa mwaminifu katika nyakati zote za maisha yako

8. KUWA MTU UNAYEUDHI KILA WAKATI.
Inaweza kuwa ni mzembe, mchafu, mtu wa kuchelewa kila mahali, mtu wa kusahihisha kila kitu mwenzio anafanya, mtu wa kulalamika tu kila wakati kila kitu, kuwa kimya tu mwenzio akitaka muongee masuala ya ndoa au familia. Unajua unaudhi lakini unaendelea kuudhi.
Usijione mbabe sana kwa sababu unayafanya hayo n mwenzako  anakuvumilia usimchukulie poa . mheshimu sana mwone n wa thamni usiendelee kuumiza kwani kadri unaumiza unasababisha mpasuko mkubwa mbeleni

9. KUWA MCHOYO.
Yaani unatumia pesa nyingi sana kwa mambo yako na mume wako au mke wako akitumia pesa kidogo tu kelele na zogo hadi nyumba inakuwa moto.
Hadi nyumba yako haipo friendly maana hata kuburudika kwa soda tu kwako ni issue wakati ukiwa mwenyewe unajichana ile mbaya na kuku kwa chips na kitimoto na watu ambao ni nje na familia yako, hiyo ni aibu!

10. UKALI ULIOPITILIZA.
Kila mwanandoa anahitaji kuwa mstaarabu linapokuja suala la kutatua mgogoro wowote, wapo ambao tatizo likitokea mke au mume na watoto wanatamani kuhama nyumba maana hapakaliki, Ni kweli kwa kelele zako na mihasira yako unaweza kuwin huo mgogoro lakini mbele ya safari bado utajikuta ni wewe ndo umeharibu zaidi.
Sidhani kama kuna mtu anapenda kukaripiwa kama mbwa ndani ya ndoa.
Jifunze kuangalia pahala pa kumkaripia mwenzako sio kila sehemu wewe unakaripia tu mbele za watoto mbele za watu wewe n wa kukaripia tu hapana kuwa makini sana hili linaua moyo wa MTU anatembea ndio ila ameshaisha ndani kwa ndani

Epuka haya ndoa yako iwe ya amani

UNAYAJUA HAYA .....
Ni imani yangu mu wazima . Nimefanya  uchunguzi kidogo na  leo nimeona tushirikishane juu ya jinsi wanawake au wasichana walivyo katika eneo la mahusiano.
Mambo haya kwa hakika yataweza kuwa chachu ya kumfanya mwanadada huyu kutoona umuhimu wa kuwa nawe au akaona umuhimu wa kuwa na wewe. Yote mawili yanawezekana .
Kwa maneno mengine yanaweza kuwa ni sababu ya yeye kukuacha na kumtafuta mwingine pale tu.

1. Anapokosa attention yako. Wasichana hupenda pale wanapofahamu kuwa unawasikiliza na unafahamu nini wao wanahitaji. Kama kutakosekana mawasiliano mazuri na atagundua hilo atauona uhusiano huo haumtimilizii haja zake. Hata kama kila kitu kinaenda sawa. Msikilize anapoongea. Kama akiona hapati penzi analolihitaji atatafuta mwingine ambaye yupo tayari kumtimizia.

2. Kumuheshimu. Msichana huwa anajitoa sana awapo katika mahusiano hivyo anategemea mvulana uheshimu hata kwa chochote kidogo anachokufanyia. Mfanye agundue kuwa umeheshimu kile ambacho amekufanyia.

3. Usaliti. Unaposaliti inamaanisha kuna kitu hakipo sawa katika mahusiano yako hata kama una uwezo wa kushughulikia lakini wewe unaona njia sahihi ni kutoka nje kuwa na mahusiano na msichana mwingine ukidhani ndio unarekebisha. Pale msichana wako akikukamata unamsaliti fahamu hawezi kuvumilia naye atakuacha.

4. Ukosefu wa hisia za kimapenzi. Msichana hupenda kuona kuwa wanapendwa wanathaminwa na wapenzi wao. Wanawajali sasa wakiona kuwa hakuna conection ya hisia za kimapenzi kutoka kwa mvulana wake huona kuwa hakuna mapenzi ya kweli katika uhusiano aliopo.

5. Unapomcontrol sana. Msichana hupenda mvulana atakayemlinda na kujiona yupo sehemu salama sio kumdhibiti kufanya mambo yake mengine anapenda uhuru. Uhuru huu ni ule utakao leta afya katika mpenzi yenu

6. Wasichana / wanawake  wengi ni wepesi wa kujiamini pale wanapokuwa mbele za wapenzi wao wakijua kwamba wewe mwanaume unaweza kufanya lolote kwa ajili yake. Anaweza hata kumkaripia konda akijua kuwa wewe uko kwa ajili yake kumlinda . Sasa ukianza na wewe kumkaripia mbele ya watu na kutomwonyesha kuwa unauwezo wa kumlinda basi unampoteza. Mwanaume ameumbwa kumlinda mkewe /mpenzi wake

7. Msichana anapokupenda sana akili yake na hisia zake zote zinakuwa kwako , anacho hitaji ni kumuonesha kuwa unamjali na unazielewa hisia zake. Unapoonyesha kutokujali na kudharau unauumiza moyo wake na kufanya awaze juu ya mwingine anaye weza kufanya hivyo hata kwa maneno tu. Anapotokea anayeweza kumjali na kumhurumia. Ukishindwa hivyo hakika jua tu kuwa umeshamkosa
kwa leo tuishie hapa........ Share kwa wenzako pia wayajue hayo.

KIJANA UNAYAJUA HAYA...

Labda nianze kwa kusema kuwa, tabia ya kununa nuna ni tabia ya wanawake, samahani dada zangu lakini inapendeza na inakua na raha zaidi mwanamke akinuna kidogo, tena raha akiwa mjamzito ili umbembeleleze kidogo na vizawadi, umshike na mashavu na kumkuna kuna tumbo ukiomba kamsamaha ili mambo yaishe, yanakua mahaba mwanamke akinuna kidogo, na kama ni mwanamke mwaka unapita hununi hata kidogo nawewe una matatizo.

Sasa hembu vuta picha mwanaume mtu mzima, na midevu yako ambayo imefanya kidevu kimeota mapele kama fenesi eti nawewe unanuna wiki nzima umevimbisha mashavu unataka kubembelezwa kweli? Tena mwingine una na watoto umenuna unawanunia watoto! Unaboa na ni tabia za kuelekea LEBA! Sasa kuna wanaume wa namna hii, unakuta mwanaume ndiyo kafanya kosa lakini atanuna wiki nzima ili mwanamke ajishushe na kuomba msamaha.

Mwingine hata hakuna kitu cha maana, hana pesa au ana matatizo mengine anajinunisha ili mwanamke asiombe mechi. Mwanaume kukasirika kupo, unakasirika, unafoka uantaoa hasira lakini hunini! Sasa kama dada yangu uko na mwanaume ambaye kila kitu ni kununa, usipomsemesha basi hata mwaka anaweza kununa basi nadhani Makala hii inakufaa sana. Ni lazima ujue namna ya kuishia na mwanaume wa namna hii kwani usipoangalia utachanganyikiwa sana.

(1) Acha Kuomba Misamaha Ya Kijinga Jinga; Najua wanawake wengi ni watu wa kufunika kombe ili mwanaharamu apite, ukiwa na mwanaume wa namna hii, kwakua hupendi kununiwa basi unaona  bora kuomba msamaha, hata kama kakosa yeye, umemfumania unaomba msamaha kwa kushika simu yake, kachelewa kurudi unaomba msamaha kwa chakula kilichopoa au kanuna tu hata hujui sababu lakini unaomba msamaha. Nikuambie tu acha kuomba misamaha ya kijinga jinga.

Mwanaume wa namna hii unapomjengea mazoea ya kumuomba msamaha unamuambia yeye hafanyi makosa, kila kitu kwake ni sawa, ni sawa na kumuambia “Hata ukitembea na Mama yangu mzazi ni sawa wewe ni malaika hukosei!” Mazoea haya yataleta amani kwa muda kidogo lakini yataondoa furaha ya milele. Hivyo kama unaona kabisa hujakosa au kanuna hujui kosa lako basi acha kuomba msamaha, mauche hata akinuna mwaka mzima lakini usiombe msamaha kama hujui kosa lako au hujafanya kosa.

Lakini inawezekana umemkosea na unajua kosa lako, hembu aomba msamaha mara moja mbili tatu kisha nyamaza. Narudia cha kuomba msamaha kila siku utafikiri ni sala ya asubihi, kumuendekeza hivi kunamfanya ajione kama Mungu. Atakunyanyasa mpaka basi, omba mara moja, ya pili, ya tatu iwe mwisho, muache anaune. Unaboa kama eti kanuna unaomba msamaha mpaka basi, unamfanya ajione Mungu flani wakati yeye akikosea hata msamaha haombi!

(2) Acha Kuliza Uliza Kwanini Kanuna; Wanawake wana hiki kitu, unakuta mtu kanuna zake, ana mahasira yake ambayo hayaeleweki basi wewe ni kumuuliza, mume wangu mbona umenuna, mbona uko hivi, nimekukosea, ni nini mbaya…. Yaanmi unauliza mpaka inakua kama wimbo. Iko hivi ni vizuri ukimuona mwenza wako hayuko sawa kumuuliza matatizo yake, lakini ukishauliza mata  mbili basi,. Kama hajakuambia muache aendelee kununa zake.

Unataka nini sasa, kama mtu yuko kwenye siku zake za kununa inakuhusu nini, muache anune baada ya muda atajiona fala ataacha. Lakini ukimuuliza kila saa anakua kama litoto, ni kama mtoto mdogo, akilia bila sababu kama ukimpuuza basi atakaa atanyamaza na kuona anchofa nya ni ufala, lakini kama ukimuuliza uliza kila saa basi jua hatanyamaza, atataka kubembelezwa. Hivyo kama mume wako kanuna  na hasemi sbabau muache anune zake hata mwaka usiulize ulize kila saa unamjengea ufala kichwani kwake.

(3) Usinune Naye, Endelea Na Maisha Kama Kawaida; Watu wa namna hii wanataka ubebe visirani vyao, eti yeye kanuna, umekosea au kakukosea au hata hujui kanuna nini? Eti anataka nawewe unune, usiangalie TV, usitoke, usisikilize umbea, usifanye chochote na hata usicheke kwakua yeye kanuna. Dada yangu kama unataka mwanaume wa namna hii anune mpaka makaburi ya Babu zenu yatikisike basi nuna naye. Kwamba eti kanuna basi nyumba nzima mpaka watoto hamna raha, basi habadiliki.

Lakini kama kanuna, kakaa na mashavu yake kavimbisha lakini wewe unacheka na watoto, uko inasta unasoma umbea na kucheka unacheka, tena wakati mwingine wakati unaangalia SULTAN unasukuma Rimoti makusidi karibu yake kisha unamuambia naiomba asipokupa unanyanyuka na kuichukua bila kulalamika wala kuuliza kwanini umeninyima rimoti…kwanini hivi kwanini vile basi atachoka na kuacha kununa. Anatakiwa kufahamu kuwa kununa kwake wala hakubadilishi chochote.

Acha kuwa na kisirani kama yeye, uantakiwa kujua kuwa mwanaume wa namna hii anafanya makusudi kununa, kwa maana kuwa ananuna ukiwepo akitoka kazini anafuraha kabisa, akiwa na watu wengine ancheka kabisa ila ukiingia wewe ndiyo kisirani kinaanza. Kwa maana hiyo kama ukinuna naye utajikuta unachanganyikiwa wewe kwakua mwenzako yeye wala hajanuna kikwelikweli, unajikuta unakua na kisirani wewe unakoda wakati mwenye rohombaya ni yeye, hivyo acha kununa naye, akinuna wewe endelea na maisha yako kama vile hayupo.

(4) Nuna Akikuudhi; Wanaume wa namna hii kwanza wanajiona kama malaika, wanajiona kama vile hawakosei, mara nyingi hawaombi misamaha na hata wakiomba basi watataka wewe usahau dakika mbili. Wakati wewe ukimkosea atanuna wiki nzima lakini yeye akikosea nataka dakika tano umsamehe na uchanganke hata kama kosa ni kubwa namna gani? Lakini pia wanawake wenye wanaume kama hawa nao wanakua si watu wa kununa, washazoea kununiwa kiasi kwamba hawawezi kununa!

Sasa nikuambie dada yangu kama mwanaume wako ni wanamna hii, mashavu kuvimba hembu jifunze na kununa kidogo. Akikukosea usiwe mwepesi wa kumsamehe, hata kiomba msamaha hembu nuna hata kwa masaa mawili, lengo sikuwa na kisirani lakini lengo nikumuonyesha kuwa yeye ni binadamua ankosea lakini kumuambia pia wewe si mti unahisia na unaumia pia. Najua unawaza vipi asipoomba msamaha si nitanuna miaka kumi?

Ishu sio yeye kuomba msamaha, hapana na wala hutakiwi kununa kwa muda mrefu, ishi ni yeye kuona tu kuwa kumbe nawewe unakereka. Asipoomba smamaha wewe endelea na maisha yako, potezea usikumbushie kosa lakini tayari atakua kajua kuwa wewe si wakupelekwa pelekwa. Usimuombe msamaha kwa kosa lake na kama akikasirika kwakua umenuna basi pia usiombe msamaha kwakua tu umenuna nayeye akanuna kwakua umenuna, hapana mpotezee na rudi katika hali ya kawaida kimya kimya, muhimu usindune muda mrefu kama yeye, masaa mawili matatu yanatosha.

(5) Tengeneza Furaha Yako Mwenyewe Ambayo Haimhusu; Hiki ni kitu ambacho wanawake wengi wanakishindwa. Wanawake wenye wanaume kama hawa wanakua kama vile wanawashwa, yaani ni kama wanayaka kuongea na hao wanaume kila saa, wakinuna nawao wanakua hawana kitu cha kufanya wanajikuta hawana raha nakuwa kama wamenuna. Hii ndiyo hupelekea wengi wao kuishia kuomba misamaha isiyo na kichwa wala miguu. Sasa kama mwanaume ni lazima kujifunza kutengeneza furaha yako wewe mwenyewe.

Najua kwakua umbahili nikikuambia ununue Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu”usome sehemu ya nne namna ya kujitengenezea furaha yako utalalamika mpaka pale ndoa imeshindikana ndiyo utanunua ila niseme tu soma sehemu hiyo. Lakini kwa wale wabahili kabisa nisem, kujitengeneze furaha yako mwenyewe ni kujifanyia mambo ambayo ungetamani kufanyiwa na mtu mwingine lakini hakufanyii, unajifanyia wewe mwenyewe na unakua na furaha yako.

Hembu tengeneza orodha ya vituambavyo ungependa mume wako akufanyie, siku akinuna jifanyie, hata kama ni kujisifia jisifie, jinunulie zawadi, jitoe out, jipikie chakula kizuri, ongea na marafiki na vingine vingi. Kwamba wakati kanuna usisimamishe maisha yako, yaache yaendelee na muache na mnuno wake, nina uhakika utakua na furaha na baada ya muda atajiona fala kwa kununa nuna bila sababu. Ataacha hiyo tabia kwani ataona anajiumiza mwenyewe wakati wewe wala ndiyo unanenepeana kama umeshinda BIKO!

NAMNA YA KUISHI NA MWANAUME AMBAYE ANA TABIA YA KUNUNA NUNA