Social Items

PropellerAds

KACHUMBARI

Ukiona mwanaume anajiweka mbali na wewe, mko sehemu moja lakini anaweza kukaa hata miezi mitatu hataki kuonana na wewe. Kila mkipanga kuonana anatafuta sababu ya kutokuonana na wewe, hajali kuhusu wewe na usipomtafuta anaweza kukaa hata wiki mbili hakupigii simu na akikupigia wala hajali kama unaendeleaje, yaani mtu ana muda hajakutafuta lakini akikutafuta anajifanya kama mliongea naye jana basi jua kuwa huyo si mpenzi wako.

Huyo ni mwanaume wako ambaye mara kwa mara akiwa na shida, akitaka kubadilisha mboga anakutumia kingono tu lakini hakuna upendo hapo! Hakutaki na ashakuambia kuwa hakutaki ila kwakua wewe ni king’ang’anizi na rafiki zako hawataki kukuambia ukweli ndiyo maana unazidi kupoteza miaka na huyo mwanaume ukisema ni mpenzi wako. Dada yangu huyo mwanaume ana mpenzi wake na wewe ni kama kachumbari tu!

Kwamba katika chakula kitu cha muhimu ni chakula chenyewe, hiki utakula kila siku, lakini kachumbari ni kitu cha mara moja moja, kinaongeza utamu lakini huwezi kutengeneza kila siku kachumbari, unafanya ukijisikia mara moja moja. Kwamba huyo mwanaume hawezi kuwa na wewe, wewe si mpenzi wake anakutumia mara moja moja akijisikia,a nakupigia simu mara moja moja akijisikia, anakutoa out mara moja moja akijisikia kwakua anataka kubadilisha ladha,a nataka kachumbari tu ila mtu huyo ana msosi wake!

Najua umenielewa ila hutaki kukubali kuwa ushaachwa, unawaza “Mbona nikikaa kimya ananitafuta, mbona ananiambia ananipenda, mbona kashajitambulisha kwetu!” Dada yangu unajipa tu moyo lakini mwanaume anayependa kwanza anakua na wivu anajua kabisa kwamba nisipomjali na kumtafutatafuta hata mara mbili tatu, nisipomkunja vizuri basi atajaliwa na kukunjwa na wengine hivyo ni lazima ahakikishe mnaonana, ila kama anakuacha tu miezi hajui hata unaendeleaje, dada wewe ni KACHUMBARI.

No comments