Social Items

PropellerAds

Hii ni zawadi yangu kwako leo .

Je, wewe ni mtu ambaye unafanya jambo halafu baadaye  ukuulizwa kwa nini umelifanya ukawa na majibu mawili tu; ‘sijui’ au ‘si kina fulani ndo wamefanya’. Basi kuna majina mawili ambayo hawa watu huitwa mtaani, kama si bendera fuata upepo, basi ni boya (huwa linafuata maji yanapokwenda).

Yaani wewe mwenyewe huna sababu binafsi ya kufanya mambo unayofanya zaidi ya kuona wengine wamefanya ukafuata mkumbo tu. Ukiona mtu anafanya mambo dizaini hiyo, huyo hajitambui!

Tuulizane hapa leo kiroho safi tu; hivi unajitambua? Kama unadhani unajitambua endelea kujinoanoa hapa, ila ukiacha kusoma huu mchongo wewe ndo bado hujajitambua kabisa. Ngoja leo tupeane maujanja kuhusu kujitambua.

Kujitambua ni nini?

Basi hapo warembo mshashika vioo mnajiangalia, sio kujitambua sura, ni deep zaidi.

Ni kufahamu tabia zako, hisia zako, nguvu na udhaifu, jinsi unavyofikiri na kutatua mambo, ambavyo vyote kwa ujumla wake vinatengeneza ‘image’ yako ya jinsi unavyojichukulia na kuwachukulia wengine pia.

Kujitambua hutusaidia kufanya maamuzi sahihi ya jinsi ya kukabiliana na misukumo mbalimbali toka kwa marafiki zetu, ndugu, jamaa na mazingira yanayotuzunguka.

Dalili za upungufu wa kujiamini

Mtu asiyejiamini mara nyingi hushindwa kujitegemea kimaamuzi na kusubiri watu wengine wamuamulie. Hiyo ina maana huna maamuzi binafsi huna msimamo. Hiyo hupelekea kutoheshimika kwenye jamii inayokuzunguka. Na kwa maana hiyo basi hata mahusiano na watu huwa mabovu.

Jinsi ya kujitambua

Kujitambua ni ujuzi. Hii ina maana kuwa unatakiwa kujifunza jinsi ya kujitambua na kufanyia kazi ujuzi huu kila siku ili uweze kuwa mkali wao katika masuala ya kujitambua.

Kwa nini kujitambua ni muhimu?

• Ni tabia ambayo inasaidia kutatua changamoto za kimaisha.

• Kuweza kuelewana na watu.

• Unaweza kujenga mahusiano bora kati yako na familia na marafiki.

• Inasaidia kutatua matatizo ya kimahusianobadala ya kuweka chuki na kinyongo kwa watu, zzunaongea nao na kutatua migogoro.

• Moyo unakuwa na amani hata wakati wa matatizo makubwa, kwani unakuwa na uhakika wa jinsi ya kuweza kuyatatua.

• Unafukuzia mbali ‘stress’ zote zisizo kuwa na tija yoyote katika maisha yako.

• Unajijengea kujiamini na uwezo wa kuwapotezea kwa urahisi wale wote ambao wanajaribu kukuletea matatizo katika maisha yako.

Ili kujitambua inatakiwa:

1. Kuwa na maamuzi binafsi. Fanya unachojisikia kufanya pasipo na nia ya kuwaumiza wengine au kuvunja sheria lakini bila ya kufuata mkumbo wa wengine wanachokifanya. Mfano: Kama washkaji zako wanapanga kwenda sehemu, na wewe hujisikii kwenda usilazimishe kwenda na wala usione aibu kuwaambia ukweli.

2. Chukua muda kutafakari kuhusu maisha yako ulipotoka, hapo ulipo na unapotaka kuwa na njia gani zitakusaidia kuwa bora zaidi.

3. Kuwa muwazi katika mambo unayoyafanya.

4. Usipende kuhukumu watu haraka kutokana na vitu wanavyovifanya bila kujua ni nini kilichowasukuma kufanya wanachokifanya.

Kumbuka

Kujitambua ni ujuzi unaoweza kuupata kwa kujifunza na kuutendea kazi. Mtu anayejitambua hufanya maamuzi kwa matakwa binafsi na kwa sababu anazoweza kuzielezea. Jitambue.

Zawadi

No comments