Social Items

PropellerAds

Mwanamke na uvumilivu

Inajulikana kwa wengi kuwa mwanamke ni kiumbe mvumilivu sana na huwa akivumilia anavumilia na kupenda kweli kweli ila ikitokea amechoka huwa harudi nyuma akisema kuwa amechoka ni amechoka na kamwe harudi tena.

Mwanamke akikupenda, lazima atakuvumilia kwa kila jambo, hadi kwa mambo yako yasiyofaa, yanayomkera, yanayomuumiza na kumtesa kihisia. Atakaa Kimya na wakati mwingine hata sema lolote zaidi ya kuitika tu kuwa ni Sawa kwake Kwa kila jambo.

Hali hii imewafanya wanaume kuendelea kumtesa na kumfanyia vituko kila kukicha huku ukidhani kuwa hawezi kukuacha na hata akikuacha lazima atakurudia baada ya siku kadhaa. Yaani hawezi kuishi bila wewe.
Huku ni kujidanganya Sana kuwa wewe tu ndio mwaname na kamwe hakuna maisha kwake bila wewe. Kauli hii huwa inawapotosha wengi sana.
Kaka zangu uvumilivu una kikomo chake.
Na usiombee mwanamke wako afikie kikomo chake cha kukuvumilia. Ukimya wake kukaa na kukuomba msamaha hata kama hajakosa usimchukulie poa ni kuwa a nakupenda na ndio maan anavumilia, ndugu akichoka hapo n hatari sana.
Akifika sehemu akachoka utajikuta na majuto, sababu mwanamke akifanikiwa kumove on, huwa harudi tena nyuma. Japo wengi wao ni wazito kuamua kuanza  na kuondoka ila akiondoka nguvu ya kumrudisha ni kumbwa san na unaweza asirudi tena. Utapata mwingine ndio lakin sio kama yeye.

Unapoona ameshaamua kujiongeza aisee zawadi, magoti, vikao, vitisho, ndumba, maombi yako sidhani kama yatafua dafu. Kumbuka kuna wakati alikuacha tu ubadilike lakini ulimwona hana jipya na mwanamke tu. Hana atakalofanya kumbe ulikuwa unajidanganya tu bure
Kama unampenda, basi acha kumfanyia vituko, acha kumtesa kihisia, acha kumnyanyasa,
acha kumuonyesha vicheche vyako na pia acha tabia ambazo zinamkera mke wako Au mchumba wako.

Acha kabisa kuumiza hisia zake wazi wazi acha umeamua kujifanyia hayo fanya huko muonyeshe heshima basi hata kidogo. Anza  kumwonyesha kama kweli unampenda.

 Kama humtaki mwache kimya kimya tu sio lazima kumwonyesha kuwa unawanawake wengi sana. Lakin pia sio kuwa wewe ni mwanaume peke yako. Ama sio kuwa wewe ndio mwanzo n mwisho wa maisha yake tu hapana kabla ya kukutana na wewe aliishi. Hivyo acha tu kumuuliza bila sababu za msingi.

Jifunze kumjali na kumthamini kabla hajaondoka kwenye maisha yako. Mwonyeshe upendo kama umeamua kuishi naye.
Mjali tu mwambie maneno mazuri mbembeleze, mfariji, anapata shida msikilize ukiweza msaidie,  kuwa mlinzi wake basi. 
Mshike mkono anapojaribu kupiga hatua ya maendeleo. 
Ukiona umuhitaji basi mwache aende zake . Kumbuka jeraha unaloliweka sasa kwake haliponi kwa haraka kiasi hicho na maumivu yake ni makali hayavumiliki. Punguza kutiririsha machozi machoni pake.
Uangalie sana usijekuta
Unapoteza dhaabu  kwa  kuokota  mawe huko njiani utakuwa umechelewa sana . kumbuka tu kuwa MAUMIVU YA MAPENZI N MAKALI MNO usiwe sababu ya yeyote kuumia mmwache aende kama humtaki
Endelea kusoma makala hizi wakaribishe n wengine pia. Huku ukishare pia kwao. Karibu sana 

No comments