Social Items

PropellerAds

KISA CHA BINTI NA MCHUMBA WAKE MFANYAKAZI WA BENKI!

Hiki kisa kimenifunza kitu ... Kutoka kwa Iddy
Binti mmoja ambaye alikuwa na mgahawa pembeni jirani kidogo na ninapoishi mara nyingi alikua na kawaida ya kuondoka katika magahawa wake na kwenda kusimamia ujenzi wa nyumba ya mpenzi wake wa muda mrefu kidogo. Walikaa kwenye uhusiano kwa karibu miaka mitano tangu binti anasoma chuo.

Baada ya binti kumaliza chuo Baba yake alimfungulia biashara ya mgahawa kwani hakutaka kuajiriwa. Mpenzi wake huyo alikuwa ni mfanyakazi wa benki flani na mambo yake yalikuwa safi, mbali na kumiliki usafiri mzuri ambao mara kadhaa nilimuona akiutumia yule binti lakini pia alikuwa na duka kubwa la nguo mjini na alikuwa akijenga.

Binti alikuwa haambiliki hasikiki, kwani jamaa alikuwa akimjali sana na ingawa hawakuwa wakiongelea sana kuhusu kuoana, jamaa kutokana na ubize wake mambo yake mengi alisimamia yule binti. Kuanzia bishara ya nguo mpaka ujenzi wa nyumba yake, binti  ingwa alikuwa hauzi lakini aliwasimamia wafanyakazi kuhakikisha wanahudumia wateja vizuri na kubwa kabisa hawamuibii mpenzi wake.

Katika ujenzi binti alikuwa akisimamia kila kitu kuanza nyumba ilipokuwa katika msingi mpaka ilipokamilika, kwani kutokana na kazi yake jamaa alikuwa bize sana. Kwakifupi binti alichukua majukumu ya mke wa yule kaka ingawa hawakuwa wakiishi pamoja.

Lakini ghafla walihitilafiana kidogo, baada ya binti kuona meseji katika simu ya jamaa ambazo hakuzielewa elewa alikasirika na kumnunia jamaa kwa wiki moja hivi, ulikuwa ni ugomvi mdogo tena wa kawaida kabisa, mwanamke alikuwa na haki ya kukasirika na alitakiwa uombwa msamaha lakini jamaa hakufanya hivyo.

Wakati binti akisubiri kuombwa msamaha, jamaa alikuja kuchukua gari lake ambalo binti ndiyo alikuwa akilitumia mara kwa mara, akadai funguo zake na binti alipojishusha kuuliza nini mbona inakuwa hivyo wakati kitu kidogo tu wamegombana, jamaa alimuambia hawezi kuishi na mwanamke wa aina ile ambaye anamnyima uhuru!

Binti alichanganyikiwa kwani katika uhusiano wa takribani miaka mitano hakuwahi kuchunguza simu ya jamaa na hata hiyo meseji aliiona tu wakati akitaka kutumia simu ya mpenzi wake kumpigia mtu mwingine na kwakuwa walikua na huru katika kutumia simu zao hakuona ishu sana.

Binti alijitahidi kuomba msamaha kana kwamba yeye ndiyo alikuwa amekosa lakini alishachelewa, kufika kwa jamaa tayari alikuwa anaishi nja mwanamke mwingine na miezi mitatu baadaye mipango ya harusi ilishaanza. Jamaa alioa na kumuacha binti akiwa haamini macho yake.

Biashara yake ilikua imesimama, alishindwa hata kuiendesha vizuri kwakua alikuwa bize akipalilia maliza mchumba, baada ya kuachwa ndiyo ikafa kabisa kwani msongo wa mawazo wa kuachwa na maisha ya kutembea kwa mguu baada ya kupoteza kila kitu kujenga maisha ya mwingine, maringo yote kwa rafiki zake, mipango yote aliyokuwa amekwishajiwekea ilififia ndani ya wiki moja.

Kwakifupi maisha ya kimapenzi aliyokuwa ameyajenga ndani ya miaka mitano yalivunjwa ndani ya wiki moja. Wanawake wengi wapo hivi wanapopenda husahau kabisa maisha yao binafsi na kuishi maisha ya wapenzi wao na wengi wao huumia wakijakugundua kua kumbe hawakua pake yako.

Katika maisha unapaswa kujua kua kama hajakuweka ndani basi huyo si wakwako na maisha yake hayakuhusu! Achana na upuuzi wa kudhani eti kwakua mpo katika umchumba basi chake ni chako! Huo ni upuuuzi ambao utakufanya kuacha kupambana na maisha yako ukisubiria ndoa ambayo inaweza isitokee.

Unachotakiwa kujifunza hapa nikuwa kuna mtu yuko na wewe kwasababu unamawazo mazuri unamsaidia kufanya mambo yake, yuko na wewe kwakuwa yuko katika kipindi cha mpito wakati akitafuta mke wa kuoa, yuko na wewe kwakua uko katika nafasi nzuri ya kumsaidia mambo yake, yuko na wewe kwasababu bado hajapata mwanamke wa hadhi yake na siku akimpata anakuacha!

Kwakifupi kuna sababu nyingi za mtu kuwa na wewe, hivyo acha kujiahidi ndoa na hata kama yeye atakuahidi hiyo ndoa basi usiwekeze kiuchumi kwake mpaka pale mtakapofunga ndoa ambapo sheria inasema mkizinguana mnagawana. Ukiangalia katika mfano wetu nikuwa jamaa hakumpenda binti, miaka mitano kuwa na mwanaume ambaye anauwezo wa kuoa lakini hakuoi ni ujinga!

Hapa namaanisha kwamba, upo na mwanaume ana kazi nzuri, mshara mzuri na maisha mazuri, mnaambiana mnapendana na kikubwa umri wake wa kuoa umefika halafu hataki kukuoa na wewe unang’ang’ania ukisubiri mungu ashushe miujiza akuoe. Ukiwa na mwanaume wa namna hiyo sisemi umuache lakini kengele iwake kichwani kuwa inawezekana natumiwa hivyo kuacha ujinga wa kuwekeza kiuchumi kwake.

Katika mfano huu huyu binti hakuachwa kwasababu ya kusoma meseji, alichwa kwakuwa jamaa alishajua sasa ni wakati wa kuoa na tayari alishakuwa na mtu wake hivyo alikuwa akitafuta sababu ya kumuacha. Mwanaume anayekupenda hawezi kukuacha kwa sbabu yoyote ile bila ya kujitathimini au kujaribu kusuluhisha.

Hata kama kakufumania atakuacha lakini kwa uchungu na kwa mchakato wa kununiana hata mwezi mmoja. Kikubwa hapa jua tu sio kwa sababu unamfanyia kila kitu kizuri nayeye anakufanyia kila kitu kizuri ukadhani ni mume wako, anakua mume pale anapokuoa basi, hata kama kajitambulisha kwenu, hata kama kashakuvisha pete anaweza kukuacha na usiambulie kitu.

Mapenzi sio pesa lakini hakuna kitu kibaya kama kupotezewa muda na mtu uliyekua ukimpenda, uliyewekeza hisia na muda wako kwake na ghafla anabadilika ukiwa huna hili wala lile. Fanya mambo yako kama wewe, faidi mapenzi yake lakini kamwe usijisahau na kuwekeza muda wako na nguvu zako katika miradi yake katika kumjenga kiuchumi.

Uhusiano pakee ambao unapaswa kuwa nao na mtu ambaye bado hamjaoana ni uhusiano wa kimapenzi na si uhusiano wa kiuchumi. Kwa maana kuwa ingawa mwili wake utakuwa ukikuhusu kama mmefikia huko lakini kamwe pesa zake na miradi yake ya maendeleo haikuhusu kabisa hivyo acha kuwekeza akili yako na nguvu zako huko, fuata maisha yako na wekeza kwako.

Kisa cha binti n mchumba wake

No comments